David Moyes amefukuzwa rasmi kama meneja wa Manchester United. Mwenyekiti wa timu hiyo, Ed Woodward aliwasili asubuhi Jumanne hii kumweleza kocha huyo uso kwa uso kuhusiana na habari hiyo.
Moyes alikuwa ameshapewa taarifa kuhusiana na hatma yake na wafanyakazi wa klabu hiyo wakati wa mazoezi. Wachezaji hawakuwepo muda huo. Tweet kutoka kwenye akaunti rasmi ya klabu hiyo imesomeka:
BREAKING: Manchester United announces that David Moyes has left the club. The club would like to place on record its thanks for the hard work, honesty and integrity he brought to the role.’
places.
Habari zilizoanza kuenea tangu jana zilieleza kuwa wamiliki wa timu hiyo, familia ya Glazer wanadaiwa kuishiwa uvumilivu kwa kocha huyo ambaye tangu aanze kuinoa imeendelea kufanya vibaya na sasa ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa Barclays Premier League. Juzi Man United ilifungwa mabao 2-0 na Everton.
Uongozi wa juu wa klabu ulikuwa umepania kumpa muda kocha huyo lakini umeona ni ngumu kuona mabadiliko kwakuwa hata wachezaji hawamwamini tena kocha wao. Ripoti hizo zinadai kuwa nafasi yake inaweza ikachukuliwa kwa muda na Ryan Giggs huku makocha wanaowaniwa kuchukua nafasi ya muda wote wakitajwa kocha wa Dortmund, Jurgen Klopp, kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal na kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti.
David Moyes |

No comments: