Willy Paul ni msanii wa Kenya ambaye anaimba nyimbo za gospel kwa mtindo wa bongo fleva. Mwishoni mwa mwaka jana aliongea na mtandao wa Bongo5 kuwa ndoto zake ni kuja kufanya kazi na staa wa bongo Diamond Platnumz sababu anamchukulia kama role model wake.
Kutokana na mapenzi makubwa aliyonayo kwa kazi za mshindi huyo wa tuzo saba za KTMA na nominee wa vipengele viwili vya MTV ‘MAMA’ na BET Awards 2014, Willy Paul ameamua kuji re-brand’ na matokeo yake yamewapa wakenya jibu la ‘Diamond wanna be’.
Willy Paul sasa amejipa jina lingine la ‘Msafi’ na ametambulisha style yake mpya ya uchezaji inayofananishwa na ya star wa mwisho wa reli (Kigoma) Diamond.
Willy Paul, Diamond na Willy Tuva
Mwishoni mwa mwaka jana mtangazaji wa Radio Citizen Willy Tuva alimkutanisha Willy Paul na Diamond Platnumz jijini Nairobi, lakini hadi sasa haijulikani kama walifanikiwa kufanya wimbo pamoja japokuwa haijulikani wawili hao watafanya wimbo wa aina gani sababu Willy anaimba gospel na Diamond anaimba muziki wa kidunia.
Mtazame hapa Willy Paul Msafi akielezea sababu za kujiita ‘Msafi’ alipohojiwa na kipindi cha ‘The Trend’ cha NTV
No comments: